Posts

Showing posts from July, 2017

Maofisa Polisi wakamatwa kwa unyanyasaji Ureno

Image
Timu nzima ya maofisa wa polisi nchini Ureno waliokuwa zamu katika kituo kimoja cha polisi wameshtakiwa kwa makosa ya kuwafungwa kimakosa, kuwadhihaki na kuwatesa watu watano weusi waliofika katika kituo hicho kwa malalamiko ya kuwekwa kizuizini kwa rafiki yao aliyetoka katika mji wa Shanty mji ulio karibu na mji mkuu Lisbon. Waendesha mashtaka katika mji huo wanasema kwamba maofisa hao wapatao kumi na nane walitumia vibaya madaraka yao kwa kuwashikilia wanaume hao, ambao wanakadiriwa kuwa na umri wa miaka ishirini, kwa siku mbili mnamo mwezi February 2015 na baadaye Kusema uongo juu ya yale waliyowatendea . Taarifa zinaeleza kuwa maofisa hao wanashutumiwa vikali kwa ubaguzi wa rangi. Makazi hayo yasiyo rasmi, yaitwayo Cova de Moura, ni makaazi ya wahamiaji wengi kutoka Cape Verde, koloni la zamani la Ureno kutoka kaskazini Magharibi mwa Afrika.

Abiria asafiri kwa ndege na mkebe wa bia pekee kama mzigo

Image
Mwanamume mmoja amefanikiwa kusafiri na mkebe wa bia pekee kama mzingo nchini Australia. Mwanamume huyo ambaye alitambuliwa kama Dean Stinson alisema kuwa rafiki yake alikuwa amependekeza hilo kama mzaha. Mkebe huo ulifika ukiwa na kibandiko na ukiwa bado haujafunguliwa kama mzigo wa kwanza katika uwanja wa Perth baada ya safari ya saa nne kutoka Melbourne Shirika la ndege la Qantas lilisema kuwa haliwashauri abiria wengine kufuata mkondo huo. Bwana Stinson aliiambia AFP kuwa alifurahi kuwa mkee huo uliwasilia salama siku ya Jumamosi. Shirika hilo halilipishi mizigo ambayo hubebwa na abiria.

Watu wawili wakwama katika shimo kubwa Brazil

Image
Kitengo cha dharura nchini Mexico kinafanya juhudi za makusudi kutaka kuwaokoa watu wawili waliokuwa wameabiri gari ambao wamenaswa katika gari ambalo lililotumbukia katika shimo lenye urefu wa kina cha mita tano . Shimo hilo lilionekana baada ya mvua kubwa iliyonyesha katika barabara kubwa iliyozinduliwa hivi karibuni ambayo ni kiungo baina ya mji wa Cuernavaca na Mexico City. Gari hilo na pikipiki vilitumbukia katika shimo hilo ambalo linadhaniwa kujitengeneza kutokana na mvua kubwa Kuingilia sehemu ya barabara kuu iliyofanyiwa ukarabati kabla ya majira ya mvua.

Watu 8 wauwawa kwenye mafuriko Marekani

Image
Mafuriko mabaya yaliyosabishwa na mvua kubwa yamesomba kidimbi kimoja cha kuogelea katika jimbo la Arizona nchini Marekani na kuwaua watu 8. Takriban wawili kati ya wale waliouawa ni watoto. Shughuli za kutafuta zinandelea kuwatafuta watu ambao bado hawajulikani waliko. Mafuriko yalitokea eneo la Cold Springs karibu na Patson Jumamosi alasiri. "Kundi la watu walikuwa wakistarehe eneo la chini la mto, alisema afisa wa polisi David Horning. Mvua haikuna inayesha eneo ambapo watu walikuwa wakiogelea Takribana watu wanne wameokolewa na sasa wanatibiwa